Blogger Widgets

Thursday, 11 July 2013

UCHAGUZI WA UDIWANI ARUSHA KUFANYIKA JULY 14,POLISI KULINDA VITUO VYA KUPIGIA KURA


 Mkurugenzi wa jiji la Arusha Sipora Liana akiwa anaongea na waandishi wa habari kuhusiana na uchaguzi wa udiwani  jijini hapa
 picha chini na juu waandishi wa habari wakiwa wanasikiliza mkurugenzi wa jiji la Arusha

Halmashari ya jiji la Arusha inatajia kufnya uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata nne  za jijini hapa ambazo ni Elerai ,Kaloleni ,Kimandolu pamoja na Themi mnamo july 14 mwaka huu uchaguzi huu mdogo unafanyika kutokana na kuairishwa kwa uchaguzi mdogo wa kata hizi katika jimbo la Arusha mjini kutokana na sababu za kiusalama.

Akiongea na waandishi wa habari mkutugenzi wa jiji la Arusha Sipora Liana alisema kuwa uchaguzi huo uliarishwa kutokana Juni 16  kutokana na mabomu yaliyopigwa siku moja kabla ya uchaguzi na mungine ukaarishwa mapema juni 30 kutokana na kutojiridhisha kwa hali ya usalama iliyokuwepo katika jiji  la Arusha.

Alisema kuwa kwa sasa maandalizi yaote yamekamilika na taratibu zote za kutangaza tena kwa wasimamizi ,wasimamizi wasaidizi pamoja na makarani zimekamilika na pia wameshapatiwa mafunzo kwa ajili ya wasimamizi hawa yameanza jana na yataendeshwa kwa muda wa siku tatu.

Aidha Sipora alisema kuwa jumla ya wasimamizi waliochaguliwa kusimamia uchaguzi ni 416 ikiwemo wasimamizi wa vituo 136 ,wasimamizi wasaidizi 135 ,makarani 136 pamoja na wasimamizi wa akiba wakiwa nane..

Pia aliwataja wananchama walioteuliwa kugombea nafasi za udiwani kuwa ni pamoja na Mwl.Emmanuel Micheel Laizer (ccm),Gilbert Bayo(CUF),Seif Shimba (CCK),Eng Jeremiah Mpiga (CHADEMA) Boidafi shirima (TLP) hawa wakiwa ni wagombea wa kata ya Elerahi ,wagombea wa kata Kaloleni ni pamoja n  Emmanuel Miliari (CCM) ,Darwesh Ramathani (CUF),Kessy Lewi(CHADEMA) pamoja na Ngilisho Pauli kutoka chama cha demokrasia makini ,waonao toka kata ya Themi ni pamoja  Victoro Mkolwe (CCM),kinabo Edmound(CHADEMA) na Lobora Ndaproi (CUF) .

Aliwataja wagombea kutoka kata ya Kimandoku ni pamaja Edna  Saul (CCM) pamoaja na Rayson Ngowi kutoka (CHADEMA) ,aidha alisema kuna jumla ya vituo 136 vya kupigia kura ambapoalisema kaloleni kuna vituo 27,elerahi 55,kimandolu 39, na kata ya themi vituo 15 .

Alisema kuwa jumala ya wapiga kura sitini elfu mia moja ishirini na tatu (60,123)wanatakiwa kupiga kura  kaloleni itakuwa na wapiga kura 12,636,Elerai  watakuwa wapiga kura 23,797,kimandulu 17,294 na Themi wapiga kura 6,396 aidha alisema kuwa wapiga kura wote wanatakiwa kufika katika vituo mapema kwani kura zitaanza kupigwa kuanzia saa moja asubui hadi saa kumi jioni ambapo baada ya hapo watafunga na askari watakuwa wanalinda vituo vyote.

Aliwataka wananchi kutimiza wajibu wao wa kupiga kura kwani zoezi hili ni muhimu huku akiwahakikishia kuwa usalama utakuwepo wa kutosha  wakati wa kupiga kura na aliwataatharisha wananchi kuwa endapo mtu yeyete atawasumbua wakiwa katika eneo la kupigia kura  watoe taarifa kwa askari aliopo karibu yake ili achukuliwe hatua za kisheria.


''ninawaomba kutowazingatia  wanaopita kuwaaambia msijitokeze kwenda kutumia haki yenu ya msingi za kikatiba kuwachagua viongozi wenu  pia napenda kuchukuwa nafasi hii kuwatakia wananchi wote wa jiji wa arusha uchaguzi mwema''alisema Sipora.

Alimalizia kwa kuwasihi wananchi wa jiji la Arusha kurudi nyumbani mara tu baada ya kupiga kura ili kupunguza mikusanyiko isikuwa ya lazima katika vituo vya kupigia kura huku akisisitiza kuwa hawataruhusiwa watu wowote kukaa katika maeneo ya vituo vya kupigia kura zaidi ya askari pamoja na mawakala

No comments:

- See more at: http://www.helperblogger.com/2012/06/jquery-facebook-like-box-popup-with.html#sthash.AGJhd6Gy.dpuf