PAULINHO ATAMBULISHWA RASMI TOTTENHAM HOTSPUR - EKOTTO ADAI HAMJUI KABISA
Mchezaji
wa kimataifa wa Brazil Paulinho leo ametambulishwa na Tottenham baada ya
kukimilisha uhamisho wa paundi millioni 17 Corinthians ya Brazil.
Lakini wakati mchezaji huyo akitambulishwa mchezaji mwenzie wa timu hiyo
beki wa kimataifa wa Cameroon Assou-Ekotto
ameiambia Goal.com: ' Simfahamu hata alivyo. Simjui, mie sifuatilii
habari za namna hiyo. Mfano mzuri ni miaka mitatu iliyopita,
Rafael van der Vaart alikuwa ndio amekuja mazoezini mara ya kwanza,
nilimsalimia lakini sikuwa najua kama yeye ndio Rafael van der Vaart."
No comments:
Post a Comment