Mchezaji wa zamani wa Birmingham Christian Benitez amefariki dunia leo hii akiwa na miaka 27.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ecuador maarufu kama “Chucho”, mwezi
uliopita tu alijiunga na klabu ya mashariki ya mbali ya El Jaish kwa
ada ya uhamisho wa £10million.

Benitez, ambaye alikuwa akitakiwa na Tottenham, aliwahi kucheza kwa mkopo Birmigham katika msimu wa 2009-10.
Muda mchache uliopita chama cha soka cha Ecuador kimetoa taarifa rasmi na kusema 'Chucho'amefariki kutokana na mshtuko wa moyo.
No comments:
Post a Comment