
Wakati
Premier League ilipoanza mwaka 1992, kulikuwepo na mchezaji mmoja tu
aliyekuwa na imani ya dini kiislam, kiungo wa Tottenham anayetoka Spain
Nayim. Ligi hiyo ya juu kabisa nchini England sasa ina zaidi ya
wachezaji 40 wanaofuata imani ya dini ya kiislam - na wachezaji wanaleta
mabadiliko makubwa kwenye mchezo wa soka nchini England.
Tarehe
5 February, 2012, Newcastle United ilicheza na Aston Villa kwenye
uwanja wa St James' Park na baada ya dakika 30 za mchezo huo,
Demba Ba alifunga bao kwa upande wa Newcastle. Akakimbia mpaka kwenye
kibendera na kuungana na msenegali mwenzie Cisse. Wachezaji hao wawili
wenye imani kali ya dini yao walishangilia kwa kusujudu.
Kukua kwa idadi ya wachezaji wa kiislam inazidi kukua kila siku baada nguvu ya soka kuongezeka kwenye anga ya kimataifa.
Maskauti
wa kusaka vipaji wamesambaa dunia nzima kusaka vipaji vipya na premier
league imekuwa kivutio zaidi kutokana na umaarufu na ukubwa wa mishahara
ya wachezaji.
Vijana wadogo kutoka maeneo ya Afrika Magharibi, kaskazini na hata au kwenye maeneo wanayoishi watu wenye kipato cha chini kwenye viunga vya mji wa Paris - vijana hawa sasa wamekuwa mastaa wakubwa.
Vijana wadogo kutoka maeneo ya Afrika Magharibi, kaskazini na hata au kwenye maeneo wanayoishi watu wenye kipato cha chini kwenye viunga vya mji wa Paris - vijana hawa sasa wamekuwa mastaa wakubwa.
Wanaweza
wakawa matajiri na maarufu kwa kwa sasa wakichezea kwenye vilabu vya
kiingereza, lakini wengi wao bado hawajasahau mizizi ya utamaduni wao,
kitu ambacho kinawaongoza na kuwaunganisha pamoja majaribu ya kidunia -
imani yao ya kiislamu.
Wakati
mchezaji wa ubora wa Demba Ba, ambaye aliondoka Newcastle mwaka
uliopita na kujiunga na Chelsea, anaposema kwamba ni mtu anayefuata kwa
umakini imani ya dini yake, baadhi wanaweza kutoa hoja kama vilabu
vinaweza kusikiliza matakwa yao.
Wachezaji
wa kiislam wanapewa mahitaji yao muhimu yanayoendana na imani ya dini
yao - kuanzia chakula, mavazi, na pia huwa wanapewa muda wa kufanya
ibada zao - hii ni zaidi kwa wanasoka ambao bado wanakuwa wanaishi
kwenye zile academy.
Mpaka
hivi karibuni, wachezaji wote wa Premier League ambao wanashinda zwadi
ya mchezaji bora wa mechi wamekuwa wakizawadia chupa ya shampeni.

Lakini
kwa wachezaji wa kiislam, vilevi vimekatwaza. Hivyo wakati kiungo wa
Manchester City Yaya Toure alipokataa kiustaarabu kupokea zawadi wakati
akifanyiwa mahojiano kwenye Television - akisema kwamba ni kinyume na
imani ya dini yake, waratibu wa 'man of the match' ikabidi wakae na
kufikiria cha kufanya.
Shampeni iliondolewa kama zawadi na badala yake sasa wachezaji wote wanaoshinda tuzo ya 'man of the match' watakuwa wanapokea kikombe kidogo.
Wakati
Liverpool waliposhinda ubingwa wa kombe la ligi katika fainali ya mwaka
2012, wachezaji wa Liverpool wakiongozwa na nahodha wa Steven Gerrard
waliondoa nguo za daktari wa timu, ambaye ni muislam, nje ya chumba cha
kubadilishia nguo ili vilevi visije vikamwagikia nguo hizo.
Bado kunakuwepo na changamoto nyingi sana wakati waislamu wakiwa kwenye ibada ya mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Ni vipi wachezaji ambao hawali wala kunywa kwa masaa zaidi ya 12 wanaweza kucheza kwa kiwango cha juu kwa dakika 90?
Baadhi ya wachezaji
wanasisitiza kutimiza ibada ya kufunga. Wengine wanaweza kufunga wakiwa
kwenye mazoezi lakini sio kwenye mechi. Klabu zinajaribu kwa kila hali
kufuata matakwa ya imani za wachezaji wao, lakini haiwezi kuwa kipindi
rahisi kwa wachezaji au makocha.
Kiungo wa Arsenal
Abou Diaby, 27, anasema: "Arsenal wangependa mie nisifunge, lakini
wanaelewa kwamba huu ni wakati muhimu kwangu na wanajaribu kwa kila hali
kufanya mambo yaende kiurahisi."
Ba, 28, anakiri
kwamba amewahi kuwa na matatizo na makocha wake kuhusu suala la kufunga,
lakini anasema amekuwa imara kusimamia imani yake.
"Mara zote nimekuwa
na kocha ambaye amekuwa hana furaha na jambo la kufunga, nimekuwa
nawaambia: 'Sikiliza, nitafunga. Ikiwa kiwango changu bado kipo vizuri
nitaendelea kucheza; ikiwa jambo hilo ni baya basi usinipange kwenye
timu, hivyo tu.'"
Mchezaji wa zamani
wa Stoke Mamady Sidibe, 33, anasisitiza: "Kuna wachezaji ambao wanafunga
na wanafanya vizuri uwanjani, na kunakuwa hamna tatizo lolote. Kwa
upande wangu mie wakati wa Ramadhani siku ya mechi sifungi ili nisiwape
visingizio watu wengine."
Bahati nzuri kwa
pande zote mbili, Ramadhan mwaka huu inaisha August 7, siku 10 mbele
kabla ya msimu mpya wa Premier League kuanza.

Mikataba ya udhamini nayo imekuwa ikileta utata. Timu ambazo zinatangaza
biashara ya kamari na mikopo kwenye jezi zao zimekuwa zikiwaweka
wachezaji wa kiislamu kwenye wakati mgumu, kwasababu wanakuwa wanatumika
kutangaza biashara ambazo zinaenda kinyume na imani ya dini yao.
Mwezi
uliopita Papis Cisse alisema kwamba anapanga kuongea na Newcastle na
wadhamini wao wapya, Wonga, kwa sababu alikuwa na mashaka kwamba imani
yake haiwezi kumruhusu kuonekana akiwa amevaa jezi ya kuipromoti kampuni
hiyo ya kamari, pia kukawa na tishio kwamba baadhi ya wachezaji wengine
waislamu wa Newcatle kama vile Ben
Arfa, Moussa Sissoko and Mapou Yanga-Mbiwa, wangefuata mkumbo, lakini
kwa bahati nzuri hawa wengine jana walionekana wakifanya mazoezi huku
wakiwa na vizibao vyenye nembo ya Wonga, ingawa bado Cisse ambaye
hakuwepo mazoezini bado anaonekana kutokuwa tayari kuitangaza Wonga.
Golikipa
wa Wigan Ali Al-Habsi ambaye anatajwa kuwa na asili ya Tanzania
visiwani, lakini ni raia wa Oman, analizungumzia hili suala: "Sisi
wachezaji na hivi vitu vinatoka kutoka klabu, hatuwezi kufanya chochote
kuhusu suala la udhamini, tunachopaswa ni kufanya kazi yetu. Pia
waislamu wote wanajua kwamba kamari ni dhambi - hili limeandikwa kwenye
vitabu vitakatifu na pia mawaidha yanatolewa kila siku hivyo mie nikivaa
shati ya Wonga haimanishi kwamba nimesema watumie."
Mashabiki pia wamekuwa wakijifunza vitu vingi kupitia wachezaji wa kiislamu.
Baadhi ya watoto
wanaocheza kwenye viwanja vya bustani ya Newcastle wamekuwa wakionekana
wakisujudu kila pale mchezaji mwenzao anapofunga goli.
Wanaweza wasiwe
wanaelewa hasa nini kitendo hicho kinamaanisha, lakini ni ishara kwamba
matendo ya wachezaji wa kiislamu yameanza kufahamika katika utamduni wa
kiingereza.
BY AIDAN CHARLIE SEIF
BY AIDAN CHARLIE SEIF
No comments:
Post a Comment