
Ndio, inaonekana rahisi, lakini mfumo wa kukuza vipaji wa Spain upo tofauti sana ukilinganisha na England. Kwa mfano, England, watoto wanafundishwa kupiga pasi mpira unapokuwa umekabwa, lakini Spain wanafundisha wachezaji ufundi wa kuuchukua ule mpira na kuwapita wanaokukaba, na hili ndilo linalowafanya wanakuwa na wachezaji aina ya kina Iniesta - wazuri kwenye kushambulia pia kwenye kupiga pasi - mafunzo yote haya yanafanyika kupitia grass roots.

England wamekuwa na viungo wazuri sana wa kati kama vile Gazza, Lampard, Gerrard na hata sasa kinda wa Arsenal, Jack Wilshere lakini bado hawajafikia ubora wa wale wa Spain. England U21 walifungwa mechi zote za Euro ya U21, na hata England U20 haikushinda mechi yoyote katika michuano ya kombe la dunia iliyoisha hivi karibuni. Mfumo wa soka la vijana wa nchi hiyo hauendi popote japo haupo kwenye hali mbaya kama wa Tanzania. England inabidi ibadilishe - mfumo wa kusuka vipaji vya makinda upo ovyo kama ule wakubwa, inabidi mabadliko yafanyike ili siku za mbele waweze kushindana kwenye mashindano makubwa. Kitu kingine kinachowafelisha England ni kwa sababu ni wachezaji makinda kutokupewa nafasi ya kukua kiutaratibu kisoka - wamekuwa wakitumika vibaya kwa kupelekwa moja kwa moja kwenye level ya juu ya soka la wakubwa na wamekuwa wakiishia kumalizia vipaji vyao kwa kuwa majeruhi - mfano mzuri Micheal Owen. Nadhni Wilshere na Oxlade Chamberlain wangepewa nafasi ya kucheza kwenye EURO U21, kwa sababu ya kupata vizuri uzoefu na kuweza kudili na presha za mechi za mechi za kimataifa kabla ya kuchezea kwa kikosi cha wakubwa - kama ilivyo kwa Spain na akina Isco, De Gea, Illaramendi, Thiago. Na ikiwa wangefanya hivyo labda wangekuwa na nafasi ya kushinda, na ikiwa wangefanikiwa - hilo lingewahamasisha wakubwa akina Rooney kujituma na kufuata nyayo za wadogo zao.
Tatizo lingine academy za makinda hazifanyi kazi nzuri sana. Zinatengeneza wachezaji kwa matakwa/mahitaji ya vilabu na hili haliinufaishi England kama taifa. Spain na academy zao wanatengeneza wachezaji wa kihispania zaidi - mfano ni karibia timu nzima ya Spain ya wakubwa na hata zile za vijana wachezaji wake wanatokana na academy za vilabu vya nchi hiyo. lakini angalia England - ukikitoa kituo cha Luton Town Academy, ambao waliwatafuta na kukuza vipaji vya wachezaji (eg. Wilshere, Boyce, Foley etc.). West Ham pia imejitahidi kwa kuwatengeneza wachezaji kama Lampard, Rio Ferdinand na Joe Cole. Lakini hawa ni wachache sana ukilinganisha na mataifa mengine kama vile Ujerumani, Spain, Brazil, Ufaransa na hata Uholanzi.
Kwa ujumla, kuna vitu inabidi vibadilike - kwa hali ilivyo England wana safari ndefu sana ya kuweza kushindana na nchi kama Spain ambao kwa hali ilivyo ilivyo wanaonekana kuzidi kuimarika - England ipo gizani kama makoloni yake, eg. Tanzania.
No comments:
Post a Comment