
Kundi la Muslim Brotherhood limeapa kuendelea na
maandamano ya amani kupinga kuondolewa madarakani kwa Rais Mohammed
Morsi na jeshi la nchi. Wafuasi wa Mosri wamekua wakiandamana mjini
Cairo karibu na kambi kuu ya jeshi anakoaminika amezuiliwa.
Taarifa ya Brotherhood inajiri wakati kumetolewa
kibali kuwakamata viongozi wake wakuu. Hapo Jumatatu wiki hii wafuasi
wa kundi hilo zaidi ya 50 waliuawa katika makabiliano na jeshi.Ufadhili wa jeshi ungesitishwa mara moja endapo mwingilio huo wa jeshi ungelionekana kuwa mapinduzi. Hapo Jumatano maafisa wa Misri walitoa kibali cha kukamatwa viongozi wa Muslim Brotherhood akiwemo kiongozi mkuu Mohammed Badie.
Viongozi hao wamelaumiwa kwa kuchochea ghasia ambapo wafuasi wao waliuawa pamoja na maafisa watatu wa usalama. Tayari ratiba ya uchaguzi mpya imetangazwa na Rais mpya anatarajiwa kuchaguliwa mwakani sawa na bunge.
Katiba itafanyiwa marekebisho na kupigiwa kura ya maoni kabla ya mwisho wa mwaka huu.Kundi la Brotherhood limepinga mpango mpya na kuapa halitashiriki mchakato wowote bila Mohammed Morsi kurejeshwa madarakani.
No comments:
Post a Comment