Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kusambazwa
WATANZANIA wamekuwa wakitatizwa na suala la Mkongo wa Mawasiliano wa Taifa.
Kimsingi kundi kubwa la Watanzania hawafahamu Mkongo wa Mawasiliano wa Taifa ni kitu gain, kutokana na kutokuwa na uelewa wa kutosha kuhusu maana halisi na faida zake.
Baadhi ya wataalamu waliozungumza na mwandishi wa makala hii kutoka Ofisi ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwa wakati tofauti wanazungumzia kazi na faida yake.
“Hapa Tanzania mkongo huu ni rasilimali ya taifa, ni muhimu tuulinde usiharibiwe kwa kuufanya uweze kudumu kwa kutoa huduma zinazotakiwa,” anasema Adin Mgendi, Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Mawasiliano ya Simu Tanzania (TTCL).
Anasema mkongo wa mawasiliano ni njia inayowezesha mawasiliano kupita na kusafiri kwa kasi kubwa kwa kutumia mfumo wa mwanga na tabia zake halisi.
Anasema mkongo ndani una nyuzi ndogondogo ambazo zikishakatwa hazina tofauti na vipande vya chupa.
Ujenzi wa Mkongo wa Mawasiliano wa Taifa anasema unafanywa na Serikali ya Tanzania ikishirikiana na kampuni ya ujenzi kutoka China.
Anasema mradi huu kwa awamu ya kwanza ulianza mwaka 2009 ambapo baadaye ulikuja kukabidhiwwa kwa TTCL kuendesha na kusimamia shughuli zote za kiufundi na kibiashara.
Mbali ya hayo anasema TTCL wamepewa jukumu la kuuendeleza mkongo kwa maana ya kuusambaza nchi nzima kwa niaba ya serikali ikishirikiana na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.
Mgendi anasema mkongo una uwezo mkubwa wa kupitisha na kusafirisha mawasiliano ya aina zote, yaani huduma za intaneti, taarifa mbalimbali, picha za video na kuongea kwa simu kwa usikivu madhubuti.
“Mkongo unasafirisha mawasiliano kwa kasi zaidi hivyo unawezesha huduma mbalimbali ziweze kutumwa na kuonekana sehemu mbalimbali kwa wakati mmoja,” anasema Mgendi.
Aidha, Mgendi anafafanua kuwa mawasiliano yanayopita kwenye mkongo ni mazuri, hayapotezi ubora, hayana muingiliano wa mawasiliano kama inavyokuwa kwenye mawimbi ya radio.
Nini madhumuni ya ujenzi wa Mkongo wa Taifa?
Akizungumzia changamoto anasema bado mradi wa Mkongo wa Mawasiliano ya Taifa unakabiliwa na changamoto za kuifanya jamii ielewe nini maana ya Mkongo wa Taifa, faida zake na kazi zake kwa kutoa semina za kuielimisha jamii ya Kitanzania, kwa maana hiyo kunahitajika fungu la kutosha (fedha) kwa ajili ya kufanikisha hilo.
“Pia wizara husika kupitia wataalamu wa teknolojia ya habari na mawasiliano hapa nchini inapaswa kupigania na kuihamasisha serikali ili mkongo uweze kutumika ipasavyo kwenye shule, vyuo, kilimo na kwenye maeneo mengine kwa manufaa ya kuinua uchumi wa nchi,” anasema Lemunge.
Anasema ujenzi wa Mkongo wa Taifa ukikamilika utakuwa na urefu wa kilometa 10,000 na kufanya mizunguko muhimu mitatu ambayo ni kaskazini, magharibi na kusini.
Awamu ya kwanza ya ujenzi imeshakamilika kwa mzunguko wa kaskazini na sehemu chache za mizunguko mingine ya magharibi na kusini.
Anasema mkongo unaanzia Dar es Salaam kwenda Morogoro, Iringa, Dodoma, Singida, Babati, Arusha na Kilimanjaro ambapo baadhi ya sehemu umejengwa kuelekea kwenye mitambo ya TTCL katika kila mkoa ulipopita na sehemu kubwa ya mzunguko huu wa mkongo umepita kwenye nguzo kubwa za TANESCO.
Anasema mkongo unaotoka Singida kuelekea Shinyanga, Mwanza, Geita kwenda Biharamulo umegawayika kwenda Rusumo, Kabanga hadi Mutukula.
Vilevile anasema kutoka Iringa kuelekea Makambako, Mbeya, Tunduma na Kasumulo umepita katika maeneo ya mashamba na makazi ya watu.
Mzunguko wa kusini anasema unajumuisha sehemu iliyokamilika na ile iliyoungana, yaani kutoka Dar es Salaam kuelekea Morogoro, Iringa na Makambako ambapo awamu ya pili itakamilisha mzunguko wa kusini kutoka Dar es Salaam kwenda Lindi na Mtwara.
Kimsingi kundi kubwa la Watanzania hawafahamu Mkongo wa Mawasiliano wa Taifa ni kitu gain, kutokana na kutokuwa na uelewa wa kutosha kuhusu maana halisi na faida zake.
Baadhi ya wataalamu waliozungumza na mwandishi wa makala hii kutoka Ofisi ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwa wakati tofauti wanazungumzia kazi na faida yake.
“Hapa Tanzania mkongo huu ni rasilimali ya taifa, ni muhimu tuulinde usiharibiwe kwa kuufanya uweze kudumu kwa kutoa huduma zinazotakiwa,” anasema Adin Mgendi, Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Mawasiliano ya Simu Tanzania (TTCL).
Anasema mkongo wa mawasiliano ni njia inayowezesha mawasiliano kupita na kusafiri kwa kasi kubwa kwa kutumia mfumo wa mwanga na tabia zake halisi.
Anasema mkongo ndani una nyuzi ndogondogo ambazo zikishakatwa hazina tofauti na vipande vya chupa.
Ujenzi wa Mkongo wa Mawasiliano wa Taifa anasema unafanywa na Serikali ya Tanzania ikishirikiana na kampuni ya ujenzi kutoka China.
Anasema mradi huu kwa awamu ya kwanza ulianza mwaka 2009 ambapo baadaye ulikuja kukabidhiwwa kwa TTCL kuendesha na kusimamia shughuli zote za kiufundi na kibiashara.
Mbali ya hayo anasema TTCL wamepewa jukumu la kuuendeleza mkongo kwa maana ya kuusambaza nchi nzima kwa niaba ya serikali ikishirikiana na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.
Mgendi anasema mkongo una uwezo mkubwa wa kupitisha na kusafirisha mawasiliano ya aina zote, yaani huduma za intaneti, taarifa mbalimbali, picha za video na kuongea kwa simu kwa usikivu madhubuti.
“Mkongo unasafirisha mawasiliano kwa kasi zaidi hivyo unawezesha huduma mbalimbali ziweze kutumwa na kuonekana sehemu mbalimbali kwa wakati mmoja,” anasema Mgendi.
Aidha, Mgendi anafafanua kuwa mawasiliano yanayopita kwenye mkongo ni mazuri, hayapotezi ubora, hayana muingiliano wa mawasiliano kama inavyokuwa kwenye mawimbi ya radio.
Nini madhumuni ya ujenzi wa Mkongo wa Taifa?
Thomas Lemunge, ambaye ni Ofisa Biashara Ofisi ya Mkongo wa Taifa
anasema: “Kwa kutambua hivi sasa dunia imekuwa kijiji, serikali iliamua
kuingia gharama ya kujenga mkongo huu ili kurahisisha upatikanaji wa
huduma mbalimbali za kijamii kwa kutumia Teknolojia ya Mawasiliano ya
Habari (TEHAMA) kwa lengo la kuwafikia Watanzania wote.
“Kenya, Uganda, Burundi, Zambia na Malawi tayari wamekwisha kuonesha
nia na utayari wa kuwa na mkongo kama ilivyo Tanzania,” anasema.
Anasema dhumuni kubwa la ujenzi wa mkongo huu wa mawasiliano ni
kuiwezesha Tanzania kuwa kitovu cha mawasiliano kikanda, kwa kutoa
huduma za maunganisho ya mawasiliano ya ndani kwa nchi jirani.
Anasema Mkongo wa Taifa utafanikisha ufikiwaji wa malengo ya kuunganisha sehemu zote za nchi, yaani wilayani hadi vijijini.
Anasema mkongo unawezesha miradi mingine kufanikisha malengo
yaliyokusudiwa kama vile vitambulisho vya taifa na kumbukumbu za Kabidhi
Wasii (RITA).
Pia unaeneza matumizi ya huduma za TEHAMA serikalini katika kusimamia
sekta za umma kwa kutoa huduma kwa wananchi na wadau wake pamoja na
sekta za jamii na kiuchumi kwa kuongeza idadi ya wasomi na wataalamu wa
taaluma hiyo kupitia elimu mtandao.
Anasema pia una umuhimu katika kudhibiti maradhi, kwa kuimarisha
huduma za afya kwa upatikanaji wa afya ya mtandao na kuongeza uzalishaji
wa mazao kwa kutumia kilimo cha kisasa (kilimo mtandao).
Anasema pia inaongeza idadi ya watalii nchini na kuongeza kipato hivyo kuchangia kikamilifu uchumi wa taifa.
Lemunge anasema mbali ya hayo, mkongo unatumika katika kusafirisha
mawasiliano ya kibiashara, wananchi wanaweza kutuma na kupokea pesa kwa
njia ya ATM.
Pia anasema una umuhimu katika simu za mkononi kwa huduma za kutolea fedha ambazo hupunguza foleni sambamba na kuokoa muda.
Akitolea mfano mzuri wa mafanikio ya mkongo anasema yameonekana kwa
Benki ya Biashara ya NMB, ambapo utendaji kazi wa benki hiyo umebadilika
kutokana na kutumia huduma za Mkongo wa Taifa.
Vilevile anasema Mkongo wa Taifa unaifanya Tanzania kuwa kitovu cha
mawasiliano kikanda na kimataifa kwa kuunganishwa na mikongo ya
kimataifa iliyopo baharini kama ile ya Seacom na Easy, ambayo imefikiwa
Dar es Salaam.
“Tayari baadhi ya kampuni za mawasiliano ya nchi jirani
yameshaunganishwa na kuifanya Tanzania kubeba dhamana ya mawasiliano yao
kupitia vituo vyetu katika mipaka ya Kasumulo-Malawi.
“Nakonde-Zambia, Rusumo-Rwanda, Kabanga-Burundi, Mutukula-Uganda na Sirari, Namanga, Horohoro-Kenya,” anasema Lemunge.
ChangamotoAkizungumzia changamoto anasema bado mradi wa Mkongo wa Mawasiliano ya Taifa unakabiliwa na changamoto za kuifanya jamii ielewe nini maana ya Mkongo wa Taifa, faida zake na kazi zake kwa kutoa semina za kuielimisha jamii ya Kitanzania, kwa maana hiyo kunahitajika fungu la kutosha (fedha) kwa ajili ya kufanikisha hilo.
“Pia wizara husika kupitia wataalamu wa teknolojia ya habari na mawasiliano hapa nchini inapaswa kupigania na kuihamasisha serikali ili mkongo uweze kutumika ipasavyo kwenye shule, vyuo, kilimo na kwenye maeneo mengine kwa manufaa ya kuinua uchumi wa nchi,” anasema Lemunge.
Anasema ujenzi wa Mkongo wa Taifa ukikamilika utakuwa na urefu wa kilometa 10,000 na kufanya mizunguko muhimu mitatu ambayo ni kaskazini, magharibi na kusini.
Awamu ya kwanza ya ujenzi imeshakamilika kwa mzunguko wa kaskazini na sehemu chache za mizunguko mingine ya magharibi na kusini.
Anasema mkongo unaanzia Dar es Salaam kwenda Morogoro, Iringa, Dodoma, Singida, Babati, Arusha na Kilimanjaro ambapo baadhi ya sehemu umejengwa kuelekea kwenye mitambo ya TTCL katika kila mkoa ulipopita na sehemu kubwa ya mzunguko huu wa mkongo umepita kwenye nguzo kubwa za TANESCO.
Anasema mkongo unaotoka Singida kuelekea Shinyanga, Mwanza, Geita kwenda Biharamulo umegawayika kwenda Rusumo, Kabanga hadi Mutukula.
Vilevile anasema kutoka Iringa kuelekea Makambako, Mbeya, Tunduma na Kasumulo umepita katika maeneo ya mashamba na makazi ya watu.
Mzunguko wa kusini anasema unajumuisha sehemu iliyokamilika na ile iliyoungana, yaani kutoka Dar es Salaam kuelekea Morogoro, Iringa na Makambako ambapo awamu ya pili itakamilisha mzunguko wa kusini kutoka Dar es Salaam kwenda Lindi na Mtwara.
No comments:
Post a Comment