Inafurahisha kuona kuwa wapo wafanyabiashara wengi jijini Dar es Salaam wanaouza juisi ya miwa. Kimsingi juisi hii ni sukari halisia ambayo haijachakatwa. Sukari halisia ni nzuri kwa mwili kwani ina virutubisho na madini kwa wingi.
Miwa ina faida nyingi kiafya. Juisi ya miwa
inafahamika na wataalamu wa afya kwa kuwa na uwezo wa kuupa mwili nguvu
kwa sababu ya ‘glucose’ iliyopo.
Kijiko kimoja cha juisi ya miwa, kina kalori 11.
Madini halisi na vitamin zinazopatikana katika sukari ni kama
phosphorus, calcium, madini ya chuma na potassium.
Si hivyo tu, miwa ni jamii ya tunda lenye alkali
hivyo lina uwezo wa kupambana na saratani hasa ile ya kibofu cha mkojo
na saratani ya maziwa.
Miwa ina upekee wake kwani ina uwezo wa kuongeza maji mwilini, inaupooza mwili na kuupa nguvu.
Virutubisho vilivyopo katika miwa vina manufaa
makubwa katika kusaidia utendaji kazi wa ogani muhimu kama figo, moyo,
ubongo na viungo vya uzazi.
Pia, wagonjwa wa kisukari wasihofie sukari iliyopo
kwenye miwa kwani haina madhara yoyote kwao. Uzuri wa juisi ya miwa ni
kuwa sukari yake ni halisia.
No comments:
Post a Comment