
Naibu waziri wa mawasiliano nchini Ghana Victoria
Hammah ameachishwa kazi baada ya kunukuliwa akisema kuwa atasalia katika
siasa hadi atakapo pata fedha kiasi cha dola milioni moja.
Anaonekana katika kanda ya video akisema kuwa
ukiwa na pesa unaweza kuwashawishi watu. Bi Hammah bado hajatoa tamko
lolote kuhusiana na mkanda huo wa video au hatua ya kufutwa kazi.Baada ya uteuzi wake baadhi ya wadadisi walionya kuwa ana umri mdogo sana kuweza kuhudumu katika serikali.
Mwezi Agosti alinukuliwa akisema kuwa kuna shinikizo za kumtaka aibe fedha za umma kwa kuwa watu hudhani kwamba yeye ni tajiri kwa sababu ya wadhifa wake wa uwaziri.
Katika kanda hiyo alisikika akisema kuwa hatatoka katika siasa hadi atakapopata dola milioni moja.
Pia alisikika akimkosoa waziri mwenzake akisema hana akili,ana sura mbaya na anapenda sana kujigamba na kuwafokea watu
No comments:
Post a Comment