WAKATI matumaini ya Waingereza kutwaa Kombe la Dunia mwakani yakilala kwa Wayne Rooney, kiungo wa Chelsea, Andre Schurrle, ameibuka na kudai kwamba nyota huyo asingepata namba katika kikosi cha sasa cha Ujerumani.
England na Ujerumani zinaingia uwanjani leo
Jumanne kucheza mechi ya kirafiki ikiwa ni mwendelezo wa upinzani mkali
baina yao na tayari Schurrle ameanzisha vita ya maneno kwa kuichimba
timu ya taifa ya Ujerumani.
“Rooney ni mchezaji mzuri, lakini tuna wachezaji
wenye ubora sana, katika kila nafasi tuna wachezaji wawili wenye ubora.
Sijui kama angeweza kucheza,” alisema nyota huyo mpya wa Chelsea. Hata
hivyo, baadaye Schurrle alituma maoni yake katika mtandao binafsi wa
mawasiliano wa Twitter akisema: “Hilo si nililomaanisha kuhusu Rooney,
ni mchezaji mkubwa.”
No comments:
Post a Comment