Blogger Widgets

Monday, 5 August 2013

Mke wa mtu apigwa nusu ya kufa abebwa na tolori kupelekwa kituo cha polisi

                                  Akipewa kipondo
                                                akiwa nyang'anyang,a kwa kipondo

                                         Akiwa amezimia
NDANI ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, jimama mwenye hadhi yake ambaye ni mke wa mtu aliyetajwa kwa jina moja la Mary au Mama Gilo, mkazi wa Sinza jijini Dar amekula kichapo cha kutisha almanusra apoteze uhai baada ya kunaswa akiiba nguo kwa ajili ya Sikukuu ya Eid El Fitr.
TATIZO NGUO ZA SIKUKUU
Tukio hilo la aibu lililoshuhudiwa na shushushu wetu lilijiri katika moja ya maduka makubwa ya nguo Kariakoo, Dar mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mama Gilo ambaye anafahamika Kariakoo na Sinza, alinaswa akiiba nguo za sikukuu ikiwa ni pamoja na ‘madira’ ya kumalizia mfungo.
TAMAA MBAYA
Katika tukio hilo lililokusanya kadamnasi, mwanamke huyo alipigwa chabo kwenye duka la mfanyabiashara Rehema Kessy ambapo alidai kuwa alifika Kariakoo kwa lengo la kununua madira lakini alijikuta akiingiwa na tamaa ya kuiba ndiyo akanaswa.
KABLA
Awali, kabla ya kuwekwa chini ya ulinzi na raia waliokuwa na hasira kali, mwanamke huyo alidaiwa kukwapua mkoba wa mwanamke mwenzake na kujichomeka kwenye maduka kumkwepa aliyemuibia ‘pimajoto’ lakelinalodaiwa kuwa na vitu ndani yake
KIPIGO
Baada ya kutiwa mikononi ndipo watu waliokusanyika wakauliza: “Na tumfanye nini mwanamke huyu?”
Watu wakapaza sauti wakisema: “Kwa utaratibu wetu hapa Kariakoo kwa mwizi yeyote, hakuna adhabu nyingine zaidi ya kusulubiwa hadharani.”
Ndipo ikaamriwa asulubiwe kwa kupewa bonge la kipigo na kufanya watu kutanda kwenye duka hilo kwa muda wa saa nzima bila kutoka, wakitaka aachiwe ili wamalize kazi yao ya kumtoa roho kama adhabu ya mwizi anapokamatwa Kariakoo.
Katika kusulubiwa huko, Mary alikuwa akilia kwa uchungu mkubwa akisema: “Naombeni mnisamehe, nimekuwa nanyi siku zote tukifanya biashara ya madira, leo mnaniua? Naombeni mumpigie simu mume wangu baba Gilo aje anisaidie.”

No comments:

- See more at: http://www.helperblogger.com/2012/06/jquery-facebook-like-box-popup-with.html#sthash.AGJhd6Gy.dpuf