
-Mo mjasirimali kijana mwenye mafanikio ya kipekee katika bara la Afrika.
Na Mwandishi Wetu
Mjasirimali mchapakazi na Mbunge Kijana
nchini Tanzania, Mohammed Dewji (MO) ametajwa katika jarida la Kimataifa
la mabilionea duniani katika Nyanja za biashara (Forbes Africa
Magazine) kama mjasirimali mwenye umri mdogo mwenye mafanikio ya kuigwa
hapa Afrika na duniani kwa ujumla taarifa la Jarida hilo limeeleza.
Kwa mujibu wa taarifa hizo toka kwa
Jarida hilo la Forbes African Magazine linasema amekuwa Mtanzania wa
Kwanza kupata kuhojiwa na (Forbes Magazine) mafaniko, changamoto na
matatizo kadhaa kwenye uwanja wa biashara kwenye ukanda huu wa Afrika
Mashariki na kati.
Mo akihojiwa na Jarida hilo alisema toka
kwenye masaa mia moja kwa wiki na kutengeneza faida ya Millioni 85 dola
za kimarekani! Ni mafanikio makubwa katika biashara Afrika.
Anasema ni safari ya takribani miaka 12 ya ushindani wa kibiashara ndani ya mipaka ya Tanzania na Afrika kwa ujumla.
“Nani anaweza kufikiri kwamba tunaweza
kubadilisha biashara yetu toka Millioni 30 za kimarekani hadi dola
Billioni 1.1 ndani ya miaka 12 tu,’ alinukuliwa akisema.
No comments:
Post a Comment